JESHI LA MTU MMOJA LATIWA MBARONI DAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 3 August 2022

JESHI LA MTU MMOJA LATIWA MBARONI DAR

 


JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemtia mbaroni mtuhumiwa Gadi Daudi maarufu ‘Jeshi la Mtu mmoja’ (28) mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Julius Fredrick (22).


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumn ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amesema Gadi alimuua mwanafunzi huyo na kumpora simu yake ya mkononi.



“Tukio hilo lilitokea Julai 16, 2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.”Amesema Muliro.



Amesema Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina Julai 27, 2022 na lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza.



“Baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam,”amesema

CHANZO:HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso