AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MTOTO WAKE WA KIKE WA MIAKA 12-MANYARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 1 August 2022

AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MTOTO WAKE WA KIKE WA MIAKA 12-MANYARA



Salimu Hassan (42), Mkazi wa Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara, amehukumiwa miaka 30 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kike (12).


Hassan ametiwa hatiani kwenye kesi hiyo namba 70/2021 Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Charles Woiso.


Hakimu Woiso amesema anatoa hukumu hiyo ili iwe funzo kwa wanaume wenye tabia ya kuwanajisi na kuwalawiti watoto wao wa kuwazaa kwa kuwafanyia vitendo hivyo vya kikatili.


Amesema mahakama hiyo inamtia hatiani Hassan baada ya ushahidi wa mtoto, mama wa mtoto, Mary Hassan (50) na taarifa ya daktari wa kituo cha afya Mirerani, kuonyesha alifanya kosa hilo.


Amesema mama wa mtoto huyo, Mary Hassan ambaye hivi sasa ni marehemu, awali alitoa ushahidi kuwa Hassan alimfanyia vitendo hivyo mtoto huyo alipowaacha alfajiri kwenda shambani kununua mboga Septemba 16 mwaka 2021.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso