HASIRA ZA SIMBA ZAISHIA KWA GEITA GOLD - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 18 August 2022

HASIRA ZA SIMBA ZAISHIA KWA GEITA GOLD

KLABU ya Simba imeanza vizuri kwenye ligi ya NBC mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Geita Gold, mchezo ambao ulipigwa jioni hii katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika mchezo huo ambao ulionekana wa aina yake hasa kwa timu zote kuonesha soka safi la kushambulia kutafuta mabao.


Shangwe ziende kwa wachezaji wapya wa timu ya Simba ambapo leo wameonesha makali yao kwa kucheza kandanda safi na wengine kupachika mabao safi, mabao ya Simba yaliwekwa kimyani na Augustino Okrah ambaye lipiga free kick ambayo ilimshindinda kipa kwa Geita Gold na kutinga nyavuni.


Mpaka mapumziko Simba Sc ilikuwa mbele kwa bao 1-0,na baadae mshambuliaji wao mpya Moses Phiri kupachika bao kali ambalo liliwanyanyua mashabiki kwa furaha kwenye dimbaa la Benjamini Mkapa.


Simba Sc ilipata bao la tatu kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Clautos Chama ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati namatokeo kusomeka Simba Sc kuibuka na Ushindi wa mnono wa 3-0.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso