SABABU YA KIFO CHA MSANII ERICK HII HAPA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 18 August 2022

SABABU YA KIFO CHA MSANII ERICK HII HAPA

 


MSANII maarufu wa vichekesho, Zabogan Zabron (Sauti ya gharama) maarufu kama Erick ‘Hivyo hivyo’ amefariki dunia.


Taarifa zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa vichekesho, Tiny White, zinaeleza kuwa msanii huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.


Tiny White amesema asubuhi ya leo alipigiwa simu na ndugu wa karibu wa Erick na kumpa taarifa za kifo chake.


Ameeleza kuwa Erick alikuwa mgonjwa ambapo hapo jana aliwasiliana naye na kumueleza kuwa alikuwa amevimba mwili mzima.


Erick amefariki dunia akiwa nyumbani kwa dada yake Kibaha mkoani Pwani.


Inaelezwa kuwa wiki tatu zilizopita mchekeshaji huyo alilazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso