WIVU WA MAPENZI WASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI-DODOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 July 2022

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI-DODOMA


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dodoma, ACP Martini Otieno


Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali katika mtaa wa Msangalale, Kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma huku wivu wa mapenzi ukitajwa kuwa chanzo cha vifo hivyo.


Waliouawa ni Dominick Kigula ambaye ni dereva wa pikipiki (Bodaboda) na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Esta.


Mganga mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma, Ibenze Ernest, amesema miili ya waliowawa imepokelewa na kuhifadhiwa hospitalini hapo.


Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dodoma, ACP Martini Otieno, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo huku akisema wanaendelea na jitahada za kumpata mtuhumiwa.

Chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso