RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA JIJINI DODOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 July 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI SIKU YA MASHUJAA JIJINI DODOMA





RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa kitaifa itakayo adhimishwa Julai 25,2022 jijini Dodoma.


Hayo yamesemwa leo Julai 25,2022 na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo.


Mtaka, amesema kuwa mkoa wa Dodoma umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa kitaifa ambayo hufanyika kila mwaka Julai 25.


“Mwaka huu mkoa wetu umepewa heshimia kuwa ya kuwa mwenyeji kwani ipo mikoa mingi nchini ambayo inavyoviwanja kama hivi vya mashujaa hivyo nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma pamoja na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi siku hiyo ”amesema Mtaka


Amesema Wakazi wa Dodoma wajiandae kujumuika katika kushiriki siku ya sherehe ya Mashujaa ambapo pia Sherehe hiyo itaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


“Sherehe za mashujaa kitaifa zinafnyika Dodoma na Rais samia atakuwa Mgeni rasmi siku hiyo hivyo tujiandae kujumuika na Rais wetu kwenye siku hiyo Muhimu”,amesema


Hata hivyo ameipongeza kamati ya taifa ya maandalizi ya tukio hilo kwa namna ambavyo imefanikiwa kukamilisha maandalizi ya maadhimisho hayo kwa asilimia kubwa.


Ameongezea kuwa tarehe 24 Juli,2022 Saa sita kamili usiku amewataka Wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa kufika katika uwanja wa mashujaa wakati wa tukio la uwashaji wa Mwenge.


“Niwaalike Wananchi wote siku ya tarehe 24 Juli, 2022 tufike katika viwanja vya mashujaa kwaajili ya kuwasha mwenge na na sisi viongozi wa Mkoa tunaendelea na maandalizi mpaka kufikia siku hiyo”,amesema


“Mimi nitawaongoza katika tukio hilo la uwashaji wa Mwenge na tarehe 25 Juli 2022 Saa sita usiku Mwenge utazimwa na Mstahiki Meya Prof. David Mwamfupe”.Amesema Mtaka


Mtaka amesema kuwa uongozi wa mkoa wa Dodoma utashirikiana na jiji na kamati ya maadhimisho ya taifa watakaa pamoja mara baada ya tukio hilo ili kuona namna ya kulifanya eneo hilo kuwa endelevu kwa kuanazisha shughuli mbalimbali.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maadhimisho ya taifa Ofsi ya Waziri Mkuu, Batholomeo Jungu amesema maandalizi ya tukio hilo yanaendelea vizuri na watarajia ifikapo Julai 25, kila kitu kitakuwa kimekamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso