WATU SITA WA FAMILIA MOJA WAUAWA-KIGOMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 3 July 2022

WATU SITA WA FAMILIA MOJA WAUAWA-KIGOMA



Mkuu wa wilaya Kigoma, Ester Mahawe


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WATU sita wa wa familia moja akiwemo bibi kizee mwenye umri wa miaka 70 aliyefahamika kwa jina la Tilifera Toyi (70) wameuawa kwa kukatwa katwa na vitu vyenye ncha kali kichwani na kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao.


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Menrad Sindano akitoa taarifa kwa waandishi wa habari alisema tukio hilo limeikumba famiilia hiyo ya watu wanane kutoka Kitongoji cha Kakonkwe kijiji cha Kiganza Halmashauri ya wilaya Kigoma na hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa kuhusiana na tukio hilo.


Kaimu Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma aliwataja wengine waliouawa kuwa ni Januari Mussa na (35) na Joel Mussa (40) ambao ni ndugu wa tumbo moja sambamba na Sara Dunia (28) ambaye ni Mke wa januari.


Pia mauaji hayo yaliwakumba ndugu wengine wa familia hiyo ambao aliwataja kuwa ni pamoja na Christina Razalo (9) na James Joel (7) huku mtoto James Januari (4) akijeruhiwa na amelazwa hospitali ya mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu.


Mkuu wa wilaya Kigoma, Ester Mahawe akizungumza kwa njia ya simu alisema kuwa tukio hilo lililotokea mida ya saa nane usiku wa leo Jumapili Julai 3,2022 kijiji cha Kiganza halmashauri ya wilaya Kigoma ambapo watu wote walikuwa wamelala.


Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika maelezo waliyopata kwa watu mbalimbali wanasema kwamba hakukuwa na purukushani zozote ambazo zimeripotiwa kuonyesha kulikuwa na shida wakati wa tukio hilo.


“Kwa sasa ni vigumu kusema sababu ya tatizo hilo kwa sababu hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na vyombo vya ulinzi na usalama vimeanza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo hivyo taarifa zaidi zitatolewa kadri tunavyoofanya uchunguzi,”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.


Katika tukio hilo wauaji hawakumgusa wala kumjeruhi mtoto Agness Januari mwenye umri wa miezi mitatu ambaye kwa sasa amehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake.

chanzo:Malunde 1 blog

1 comment:

  1. Duuuh! Hili ni balaa la aina yake,ninahisi usalama wa nchi yetu hauko imara-kuna sehemu panalegalega!

    ReplyDelete

Post Top Ad

Pages

Huheso