AKATWA SEHEMU ZA SIRI AKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE-MANYARA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 3 July 2022

AKATWA SEHEMU ZA SIRI AKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE-MANYARA



Mkazi wa Kijiji cha Orkine, wilayani Kiteto mkoani Manyara, Nanaa Mepukori (54) amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kujeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri na watu wasiojulikana.


Tukio la mwanaume huyo kukatwa nyeti lilitokea Juni 28, 2022 usiku ambapo inadaiwa kuwa alikuwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji na alipotoka nje kujisaidia akakutana na watu hao na kumkata kwa kutumia kisu.


Mtoto wa mzee huyo, Leyaseki Mepugori (26) akizungumza akiwa hospitali ameeleza kuwa alimkuta baba yake akiwa anavuja damu baada ya kufanyiwa ukatili huo.


"Nilimkuta mzee akiwa hoi, hajiwezi hata kidogo tulimpeleka zahanati lakini walitushauri kwenda hospitali ya Kiteto kwa matibabu ambapo mpaka sasa tunaendelea nayo hospitali ya Kiteto ingawa mpango uliopo sasa ni kumpeleka Dodoma kwa matibabu zaidi” amesema mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso