WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA MAUAJI YA MWENDESHA BODABODA WALIMUUA WAKAUTUPA MWILI WAKE KWENYE SHAMBA LA MAHINDI, MMOJA ALIMKODI-NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 6 July 2022

WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA MAUAJI YA MWENDESHA BODABODA WALIMUUA WAKAUTUPA MWILI WAKE KWENYE SHAMBA LA MAHINDI, MMOJA ALIMKODI-NJOMBE




Mahakama kuu kanda ya Iringa iliyokaa katika kikao chake katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mwendesha Bodaboda.


Waliohukumiwa kifungo hicho ni Elias Jackson miaka (31), Hussein Hamis miaka (31) na Olestus Mbawara miaka (51) ambapo watuhumiwa hao wamekutwa na hatia ya mauaji ya James Kahengesa mkazi wa Makambako mkoani Njombe ambae alikuwa mwendesha Bodaboda.


Akisoma hukumu hiyo leo Julai 06, 2022 Jaji Dkt. John Utamwa amesema tukio lilitokea Juni 2016 Mtaa wa Mashujaa uliopo halmashauri ya Makambako mkoani Njombe ambapo mmoja wa washtakiwa hao alimkodi marehemu, baada ya kufika eneo hilo aliamriwa kusimamisha pikipiki yake.


Amesema njama ya watuhumiwa ilikuwa kumpora Pikipiki hiyo na walimnyonga hadi kufa na mwili wake kuutupa katika shamba la mahindi na kutoweka na pikipiki hiyo kuelekea mkoani Mbeya na walikamatwa wakiwa eneo la Lujewa wakiwa na pikipiki hiyo.


Jaji Utamwa amesema washtakiwa wanatiwa hatiani kwa kuzingatia sheria chini ya kifungu cha 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo yam waka 2019.


Mawakili wa serikali (Jamhuri) wakiongozwa na wakili Matiku Nyangero wameiomba mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria kutokana na kufanya mauaji ya kukusudia huku mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Musa Mhagama wakikubaliana na maombi hayo.


chanzo:Millardayoonline

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso