NYONGEZA YA MSHAHARA ASILIMIA 23.3 MAMBO BADO HAYAJAELEWEKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 27 July 2022

NYONGEZA YA MSHAHARA ASILIMIA 23.3 MAMBO BADO HAYAJAELEWEKA



Wakati Serikali ikisema inasubiri majadiliano ya vyama vya wafanyakazi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limesema leo Jumatano Julai 27, 2022 litapeleka hoja zao kuhusu kutoridhika na utaratibu uliotumika kwenye nyongeza ya mshahara.


Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema Jana Jumanne Julai 26, 2022 kuwa viongozi wa Tucta wameomba muda kwenda kujadiliana kabla ya kuzungumza na Serikali.


“Na baada ya mazungumzo ya awali leo, viongozi Tucta wameomba wapate muda wa kwenda kujadiliana na baadaye watakuja kuzungumza na Serikali,” amesema Msigwa.


Amesema viongozi wa Tucta watakapokamilisha majadiliano yao, watakutana na Serikali ili wasikilize hoja zao na baadaye Serikali itatoa maelezo yake.


“Sasa baada ya hapo tutawaambia kilichojili kwenye mazungumzo hayo ni nini na uamuzi wa Serikali,”amesema.


Ametaka uwepo wa subra wakati Tucta ikijadiliana na kwamba nia ya Serikali ni kujenga hakuna kitu cha kuficha wala kibaya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso