MWANAFUNZI AJIFUNGULIA MTOTO CHUMBA CHA MTIHANI SIMIYU WALIMU WALIKUWA HAWAJUI KAMA NI MJAMZITO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 30 July 2022

MWANAFUNZI AJIFUNGULIA MTOTO CHUMBA CHA MTIHANI SIMIYU WALIMU WALIKUWA HAWAJUI KAMA NI MJAMZITO



Mwanafunzi wa darasa la saba, Shule ya Msingi, Kulimi, Kata ya Kulimi wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu amejifungua katika chumba cha mtihani Julai 27, 2022.


Taarifa iliyotolewa na ofisa elimu Mkoa huo, Majuto Njaga ameiambia Mwananchi Digital tukio hilo lilitokea Julai 27, 2022 wakati mwanafunzi huyo akiwa katika chumba cha mtihani.


Amesema idara ya elimu wilayani Maswa ilitoa taarifa katika ofisi yake na kueleza kwa kipindi chote cha ujauzito walimu hawakuwa wanafahamu kama mwanafunzi huyo ni mjamzito.


"Alijifungua akiwa shuleni, baada ya kujifungua ofisi ya elimu kwa kushirikiana na maafisa wa ustawi wa jamii walifika shuleni hapo na binti alimtaja aliyempa ujauzito na tayari kesi imefunguliwa," amesema Majuto.


Amesema baada ya maafisa wa ustawi wa jamii kufika shuleni hapo, mtoto alikabidhiwa kwa wazazi wake akiwa na mwanaye kwa ajili ya uangalizi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso