FACEBOOK KUFUTWA NCHINI KENYA NDANI YA SIKU SABA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 30 July 2022

FACEBOOK KUFUTWA NCHINI KENYA NDANI YA SIKU SABA





Tume ya amani ya Kenya imeipa Facebook siku saba kuondoa maudhui yote ya chuki kwenye mtandao wake, vinginevyo itajiweka katika hatari ya kusimamishwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi ujao wenye ushindani mkali. 


Tume hiyo ya Mshikamano na Utangamano, NCIC, imesema jana kuwa imetumia mapendekezo kwa kampuni mama ya Facebook, Meta, kufuatia ripoti kwamba iliruhusu zaidi ya dazeni moja ya matangazo ya kisiasa yenye maudhui za chuki.


Kamishna wa NCIC Danvas Makori, aliwaambia waandishi habari kwamba iwapo Facebook haitatii agizo hilo, watapendekeza mtandao huo kupigwa marufuku kabisa nchini Kenya. 


NCIC ni mamlaka huru ya usimamizi wa mshikamano wa kikabila, iliyoundwa baada ya vurugu za uchaguzi wa 2007-2008, ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuawa.

CHANZO:DW

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso