KUTOKA MADHABAHUNI:WAKATI WA SHEREHE WEKENI KAMATI YA KUWAHUDUMIA WATOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 17 July 2022

KUTOKA MADHABAHUNI:WAKATI WA SHEREHE WEKENI KAMATI YA KUWAHUDUMIA WATOTO

 


WAKRISTO Wakatoliki na jamii kwa ujumla,wamehimizwa kuwajali watoto  wadogo nyakati za sherehe na matukio mengine kwa kuwaundia Kamati ya kuwahudumia,badala ya kuwa na Kamati ya kuwafukuza watoto. 


Hayo yamesemwa na Padri Patrick Tibangayuka,wakati wa mahubiri Dominika  ya 16 ya mwaka C,katika  kigango cha Bugombe,Parokia Katoliki ya Kanyigo,Jimbo la Bukoba.


Na Mutayoba Arbogast,Bukoba 


Padri Tibangayuka ambaye ni mzaliwa wa Parokia ya Kanyigo,akifanya utume katika Seminari kuu ya Nazareth-Mwendakulima,Jimbo la Kahama,ambaye yuko kwenye shughuli jimbo la nyumbani.


Katika Injili Lk 10:38-19....Bwana akajibu  "Martha,Martha,unasumbuka na ufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,lakini kinatakiwa kitu kimoja tu,na Mariam amechagua fungus lililo jema,ambalo halitaondolewa"


Akinasibisha na injiii hiyo amesema ni jambo la kusikitisha sana siku hizi nyakati za sherehe na matuki mengine,kuwaona watoto  wakibaguliwa wakati wa chakula,bila kuwekewa mtu maalum mwenye upend na kujali,wala hata hawatengewi nafasi yaani banda lao,na hivyo hula kwa bahati naibu.


"Nakumbuka huko nyuma sherehe ya kuoza au kuozeshaa ilikuwa shughuli ya kijiji chote,na mngegombana na mtu ambaye huenda kwake kuchukua Mungu wa ndizi aliokuandalia,kulikuwa na upendo mkuu,watoto  tulikula,tulikunywa na kufurahi."


Amesema,sasa watoto  hawathaminiwi tena jinsi inavyostahili,badala take kamati mbalimbali zinaundwa kuwahudumia watu wazima,hakuna kamati ya watoto  na mbaya zaidi inaundwa kamati ya kuwafukuza au kuwadhibiti watoto. 


"Utakuwa mtu amechangia gharama za bia nane,na anataka 'azifute' peke yake, kumbe angepewa bia mbili,nyingine zikagharamia soda  kwa watoto. 


Naomba niwaachie hili,lila mnapoandaa sherehe  au tukio,undeniably Kamati ya kuwahudumia watoto,hao ni malaika wadogo,na kupitia furaha yao kuna kujaliwa kwingi",amesema Padri Tibangayuka.


Programu Jumuishi ya Taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto(PJ-MMMAM)inamhiza kila mdau  wa maendeleo ya jamii kuwapa umuhimu watoto  ili wafikie kiwango  kinachokidhi makuzitimilifu,kimwili,kiakili,kiroho,kimaadili na kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso