CHIPUKIZI FC WA MOTO WAANZA KWA USHINDI MICHUANO YA IDDI CUP-MSALALA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 18 July 2022

CHIPUKIZI FC WA MOTO WAANZA KWA USHINDI MICHUANO YA IDDI CUP-MSALALA

 


Michuano ya ligi ya IDDI CUP katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imezinduliwa rasmi Jana kwa kuzikutanisha timu za Stand fc vs Chipukizi fc katika uwanja wa Mnadani.

 

NA PASCHAL MALULU-HUHESO DIGITAL


Mashindano hayo yanmefunguliwa katika Kata ya Bulige kwenye Halmashauri hiyo na katika mchezo huo wa ufunguzi Stand fc ilichapwa bao moja kwa nunge na timu ya Chipukizi fc na ligi hiyo itachezwa katika Kata 18 za Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ikianza kwa ngazi ya vijiji hadi Kata.

 

Timu ya Chipukizi fc ikiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa kituo cha Polisi Busangi, Yusuph Chenge.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ambaye alikuwa ndio mgeni rasmi mkuu wa kituo cha Polisi Busangi, Yusuph Chenge Adam alisema michezo hiyo itawapa fursa vijana ya kujiendeleza kimichezo pia kuondokana na matukio ya kihalifu.

 

Michuano hiyo imedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kassim ambapo Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa Ng’ombe mmoja, mshindi wa pili shilingi laki tano na mshindi wa tatu shilingi laki tatu.

wananchi wakishuhudia mchezo wa Stand fc dhidi ya Chipukizi fc ikiibuka na ushindi wa bao 1-0

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso