CCM KURUDIA UCHAGUZI, BAADA YA WANACCM KUBAINIKA KUPANGA SAFU YA UONGOZI NDANI YA CHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 23 July 2022

CCM KURUDIA UCHAGUZI, BAADA YA WANACCM KUBAINIKA KUPANGA SAFU YA UONGOZI NDANI YA CHAMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Morogoro Mjini, kimetengua kisha kuamuru kurudiwa kwa shughuli ya uchukuaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho na jumuiya zake.


Ni baada ya kata nane kati ya 29 kubainika kuwa na dosari kwenye shughuli hiyo ya awali ya uchukuaji fomu kwa baadhi ya wagombea kudaiwa kupanga safu ya uongozi mkoani humo.


Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa, Julai 22, 2022, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Chief Sylvester Yaredi amesema kata nane kati ya 29 zitarudia uchukuaji fomu baada ya kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu CCM wilaya kujiridhisha kwa dosari nyingi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso