AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA KAKA YAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 23 July 2022

AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA KAKA YAKE




Mahakama ya Wilaya ya Muheza - Tanga imemhukumu kifungo cha maisha gerezani Paulo Mngazija (39) mkazi wa Kicheba B kwa kumlawiti mtoto wa kiume wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.


Mngazija alitenda kosa hilo kwa mtoto huyo wa miaka sita Juni 19 mwaka huu.


Kesi hiyo ya jinai namba 65 ya mwaka 2022 ilifunguliwa na kuanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza Juni 23, 2022.


Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Muheza, Yusuph Abdallah Zahoro, amesema mtuhumiwa ametiwa hatiani chini ya kifungu cha 154 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya mwaka 2019.

chanzo:Azamnews

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso