ASUSIA KUJITETEA KWENYE KESI INAYOMKABILI MAHAKAMA YATOA HUKUMU YA MIAKA 30 JELA-DAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 28 July 2022

ASUSIA KUJITETEA KWENYE KESI INAYOMKABILI MAHAKAMA YATOA HUKUMU YA MIAKA 30 JELA-DAR





Mahakama ya Wilaya ya Temeke imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Said Issa baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.


Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Jimson Mwankenja, aliyesikiliza kesi hiyo baada ya kuridhika na ushahidi wa mashtaka.


Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pekee kwa kuwa mshtakiwa alizira kujitetea baada ya hakimu Mwankenja kukataa kujitoa katika kesi hiyo.


Awali ilidaiwa kuwa Februari 15, 2021, eneo la Mkwamba, Temeke, aliiba simu aina ya Infinix mali ya Neema Masinde.


Upande wa mashtaka uliwaita mashahidi watatu, akiwemo Neema mwenyewe na kuwasilisha vielelezo vinne, huku ikidaiwa kabla ya kupora simu hiyo, mshtakiwa alimjeruhi Neema kwa kisu mkononi na shingoni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso