MWALIMU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 27 June 2022

MWALIMU AJIFUNGUA MAPACHA WANNE



Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kuanza mchakato wa kumhamishia mjini Mwalimu Judith Sichalwe mwenye miaka 29 ambaye amejifungua watoto wanne bila upasuaji.


Mtatiro ametoa maelekezo hayo alipomtembelea Mwalimu huyo katika kijiji cha Mkapunda katika Shule ya Msingi Mkapunda iliyoko kilomita 100 kutoka Tunduru Mjini ambako anafundisha.


Mtatiro amesema ni wajibu wa serikali ya Wilaya ya Tunduru kumrahisishia maisha mwalimu huyo ambaye anaweza kukabiliwa na hatari ya kushindwa kumudu gharama za maisha kutokana na idadi hiyo ya watoto wachanga kwa wakati mmoja.


Afisa Tarafa wa tarafa ya Nalasi ambako mwalimu Judith anaishi, Salumu Kijumu ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuratibu misaada mbalimbali, lakini pia amewaomba watanzania wote watakaoguswa na kazi ya malezi ya pacha hao wanne kumsaidia mwalimu huyo.


Aidha Mwalimu Judith Sichalwe amejifungua watoto wanne katika hospitali ya Wamisionari ya Mbesa iliyoko Tunduru mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso