ANAEDAIWA KUGUSHI VIBALI WIZARA YA MADINI KESI YAKE KUUNGURUMA MWEZI AGOSTI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 30 June 2022

ANAEDAIWA KUGUSHI VIBALI WIZARA YA MADINI KESI YAKE KUUNGURUMA MWEZI AGOSTI




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti Mosi, 2022 kumsomea hoja za awali (PH) Anthony Magoe (35) anayekabiliwa na mashtaka sita likiwemo la kughushi vibali vya kusafirisha madini kutoka Wizara ya Madini na kujipatia Sh1.3bilioni kwa njia ya udanganyifu.


Hiyo ni baada ya upelelezi wa kesi hilo ya jinai namba 74/2022 kukamilika.


Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga ameieleza Mahakama hiyo leo Alhamisi Juni 30, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.


Wakili Mwanga baada ya kueleza hayo, hakimu Isaya ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti Mosi, atakaposomewa mashtaka.


Kwa mara ya kwanza, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani Mei 16, 2022 kujibu mashtaka yanayomkabili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso