SPIKA TULIA ACKSON: ZIMENI MAGARI YENU MNAPOSHUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 17 May 2022

SPIKA TULIA ACKSON: ZIMENI MAGARI YENU MNAPOSHUKA



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amewataka Viongozi mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Halmashauri, Meya, Katibu Mkuu na Viongozi wengine kote Tanzania kuzima magari yao pindi wanaposhuka ili kuokoa gharama za Serikali kwenye mafuta.


Bungeni leo May 17 2022 Spika Tulia amesema: "Nimekumbushwa leo asubuhi... magari ya Viongozi ikiwa ni pamoja na Mawaziri na Manaibu Mawaziri yanaendelea kuwaka hapo nje wakati sisi tupo humu ndani, tunatamani magari ya Viongozi yakishamshusha Kiongozi sio tu hapa Bungeni bali Nchi nzima yazimwe na Dereva ashuke kwenye gari kwa sababu matumizi ya pesa kwenye eneo la mafuta yanakua makubwa sana kwa sababu ya magari kuendelea kuwaka wakati Kiongozi hayupo kwenye gari ameshashuka lakini gari linaendelea kuwaka”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso