PANYA ROAD WALIOTIKISA DAR WAPANDISHWA KIZIMBANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 17 May 2022

PANYA ROAD WALIOTIKISA DAR WAPANDISHWA KIZIMBANI




Watuhumiwa 25 wa matukio ya uvamizi na kujeruhi watu kwa silaha ikiwemo mapanga, yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam, wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne na Kitengo cha Habari cha Jeshi hilo.

Jeshi hilo limesema watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo leo Jumanne, tarehe 17 Mei 2022 na kusomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu Mkazi, Fadhili Luvinga.

“Kwa mara nyingine kundi lingine la wahalifu 25 ambao wengi wao ni vijana maarufu kama ”Panya road” waliokamatwa wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha. Walifikishwa mbele ya Hakimu Luvinga kusomewa mashtaka sita yanayowakabili,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, watuhumiwa hao walisomewa mashtaka na waendesha mashtaka wa Serikali, Wakili Michael Ng’hoboko, Avelina Ombock na Nancy Mushumbusi.

Wakiwasomea mashtaka hayo, mawakili hao wa Serikali walidai watuhumiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, tarehe 24 Aprili, 2022, 25 Aprili 2022 na 29 Aprili 2022, maeneo ya Gongo la Mboto, Kipunguni na Karakata jijini Dar es Salaam.

Waendesha Mashtaka walidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na waliomba tarehe kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

CHANZO:WATETEZI TV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso