KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA ALIYEMWAHIDI KUMUOA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 28 May 2022

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA ALIYEMWAHIDI KUMUOA

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemsomea shtaka la ubakaji kijana Faison Alimajani Sanga (19) mkazi wa kijiji cha Makwaranga kata ya Ipelele anayetuhumiwa kutekeleza kosa hilo kwa mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani humo anayetajwa kuwa na umri wa miaka 15

Mahakama imeeleza kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) e na 131 (1) ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2019.

Kwa upande wa mashaidi wawili wa mashtaka akiwemo muhanga mwenyewe amesema kuwa mnamo tarehe 12 Februari, 2022 mshtakiwa alimpeleka nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho huku akimuahidi ya kuwa atamuoa.

Shahidi wa pili ambaye ni baba wa mtoto huyo amesema kuwa alipogundua binti yake ni mjamzito na kuamua  kumpeleka kwenye kituo cha afya kwa ajili ya vipimo  na ndipo alipo gundulika ni mjazito 

Aidha mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kurejeshwa rumande mpaka tarehe 30.5.2022 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa Tena.


CHANZO:MUUNGWANA BLOG


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso