HUKUMU YA SABAYA YAPANGWA JUNI 10 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 31 May 2022

HUKUMU YA SABAYA YAPANGWA JUNI 10



Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita kutokana na Hakimu kuwa na majukumu mengine.


Akiahirisha kesi hiyo leo Jumanne Mei 31, 2022, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa amesema shauri lilipangwa kwa ajili ya hukumu ila hakimu aliyekuwa akiisikiliza amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi.


"Shauri linakuja kwa ajili ya hukumu na liko kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda lakini siku ya leo amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi hataweza kutoa hukumu leo hadi Juni 10, 2022," amesema Hakimu huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso