ALIYEBAKA MTOTO WA MIAKA 8 AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 29 April 2022

ALIYEBAKA MTOTO WA MIAKA 8 AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

 

 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe, Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa miaka 8.

 

Fadhili amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka Mtoto wa miaka 8 ambaye ni Mtoto wake wa kambo aliyekuwa akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo katika kata ya Ulembwe.

 

Inaelezwa kuwa siku hiyo Mshtakiwa alimbaka Mtoto huyo na kumwambia asipige kelele.


Hata hivyo Tarehe 23/2/2020 Mama wa Mtoto huyo alimuona Mwanae hatembei vizuri ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha Binti huyo akamwambia Mama yake kuwa Baba yake wa kambo alimbaka.

 MWISHO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso