NGAYIWA AMEISHAURI MANISPAA YA KAHAMA KUSAJILI JUKWAA LA WANAWAKE NEST - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 25 September 2026

NGAYIWA AMEISHAURI MANISPAA YA KAHAMA KUSAJILI JUKWAA LA WANAWAKE NEST





Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Benjamin Ngayiwa (kushoto) akiteta jambo na afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Kahama Elia Moshi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.


Imeelezwa kuwa uanzishwaji wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga litawaunganisha wanawake na kutafuta suluhisho la changamoto zao na kuwaunganisha na fursa za mbalimbali za kiuchumi.






Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kahama, Elia Moshi, amebainisha hay oleo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa jukwaa hilo ngazi ya Manispaa na kwamba linalo jukumu la kuwaunganisha wanawake na fursa za kupata fedha kupitia benki na taasisi nyingine za kifedha.






Ameema hatua hiyo itawawezesha kukuza shughuli zao za kiuchumi na kuboresha maisha yao.




Amesema moja ya maeneo ambayo jukwaa hilo litayapa kipaumbele ni kuwawezesha wanawake kujadili changamoto zinazohusiana na shughuli zao za uzalishaji, ikiwemo kilimo, upatikanaji wa mbegu na namna ya kuwafikia taasisi za kifedha kwa ajili ya mitaji.






“Jukwaa hili kazi yake ni kuwaunganisha kina mama katika maeneo yao, mipango yao, ili waweze kukaa pamoja na kujadili masuala yao yanayowahusu, jinsi walivyoweza na changamoto, kujua fursa na mambo mengine,” amesema Moshi.






Mbunge wa Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, aliyekuwa mgeni rasmi katik jukwaa hilo, amewashauri Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Kahama kulisajili jukwaa hilo kwenye mfumo wa Nest ili wanawake waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotangazwa na serikali.






“Kama kujisajili kwenye mfumo wa NEST, huwezi kutafuta hizi kazi na huwezi kupata hizi fursa.” amesema Ngayiwa.






Aidha amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake kiuchumi, akieleza kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika kuimarisha familia, ustawi wa jamii na kuchangia maendeleo ya taifa.






Amesema hatua hiyo inaendana na juhudi za Serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi, ikiwemo kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na kila halmashauri nchini kwenda kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.


















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso