Mfumo wa ununuzi wa umma wa kielektroniki wa NeST umewezesha vikundi 299 vya vijana vyenye jumla ya vijana 2,226 kupata zabuni za Serikali, huku takwimu zikionyesha kuwa kiasi cha fedha kilichoingia mikononi mwa vijana hao kupitia zabuni hizo kinafika shilingi bilioni 13.2.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, akizungumza jijini Dodoma katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa.
Aidha amesema Serikali imeendelea kuweka mifumo na programu za kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo mikopo, zabuni za Serikali, mafunzo ya ujuzi na matumizi ya teknolojia, hatua inayolenga kuongeza fursa za ajira na ujasiriamali nchini.
Amesema Serikali imeweka ajenda ya vijana katika msingi wa sera, uratibu na utekelezaji ili kuhakikisha vijana wanapata fursa kulingana na mazingira wanayoishi.
Amesema kupitia Youth Empowerment System (YES), vijana wataweza kujisajili, kujenga wasifu, kutafuta fursa, kuomba kushiriki katika programu mbalimbali na kutoa mrejesho, huku Serikali ikitumia mfumo huo kujenga kanzidata ya vijana na ujuzi wao.
Mafunzo haya ya matumizi ya mifumo ya kidijitali yanajumuisha pia Mfumo wa Youth Empowerment System (YES), ambao unatumika kuwasajili vijana, kujenga wasifu wao, na kurahisisha upatikanaji wa fursa kulingana na kanzidata ya ujuzi iliyopo nchini.
Mbali na mfumo wa NeST, jitihada za serikali katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia mikopo na programu mbalimbali zimeendelea kushika kasi katika mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo vijana 126 walipatiwa mikopo ya vifaa yenye thamani ya shilingi milioni 824.4 katika mikoa ya Mwanza, Mtwara, Mbeya, Rukwa, na Arusha.
Sambamba na hilo, vikundi vingine 5,199 vya vijana nchini kote vimefanikiwa kunufaika na mikopo ya Halmashauri kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 52.168.
Ili kuimarisha zaidi fursa hizi, serikali kupitia Ofisi ya Rais inayoshughulikia Maendeleo ya Vijana chini ya Waziri Joel Nanauka inaendelea kuchukua hatua za kimkakati kwa kuweka ajenda ya vijana katika msingi thabiti wa sera, uratibu, na utekelezaji.
Hatua hizi zinalenga kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya ujuzi stahiki, wanatumia teknolojia ipasavyo, na wanashiriki kikamilifu katika miradi ya kimaendeleo ili kuongeza fursa za ajira na kukuza ujasiriamali nchini kote.
No comments:
Post a Comment