WATU 23 WAPANDISHWA KIZIMBANI MWANZA KWA TUHUMA ZA MIKUTANO YA KIGAIDI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 25 July 2026

WATU 23 WAPANDISHWA KIZIMBANI MWANZA KWA TUHUMA ZA MIKUTANO YA KIGAIDI


Watu 23 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja linalowakabili la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.


Wanaotajwa kukabiliwa na shtaka hilo ni pamoja na Alphaxad Nyamwaga, Fantson Mpango, Abely Mwesa, Hassan Said, Emmanuel Wambura, Adam Idd, Damas Sadock, Petrol Mabula, Abdul Kagwidi, Devid Mahendeka, Philipo Masatu, Edward Mikindo, Emmanuel Doto, Deus Masalago, Mohamed Tosha, Fabian Nguvumali, Samwel Mtani, Samwel Kobell, Julius Makonga, Fanuel Lutana, Philipo Kulwa, Philipo Shipuluko na Hamis Mnyivua.


Washitakiwa hao, ambao baadhi yao ni viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), walifikishwa mbele ya Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Hakimu Erik Marey, na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mwanza, Jaji Ephery Kisanya, ambapo walisomewa mashitaka yanayohusiana na kujihusisha na vikao na mazungumzo yanayoweza kuhatarisha usalama na kupelekea ugaidi.


Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, inadaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya Juni 25 hadi Julai 6 mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa katika Wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza, walishiriki kukaa vikao mbalimbali vya kupanga kutekeleza vitendo vya ugaidi, ikiwemo mpango wa kuchoma moto majengo pamoja na mali mbalimbali za serikali na za wananchi binafsi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso