RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA NCHINI URUSI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 4 June 2026

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA NCHINI URUSI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Doctor Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) jijini Moscow tarehe 4 Juni 2026.


Shahada hiyo ilitolewa na Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Oleg Yastrebov, kwa kutambua mchango wa Mhe. Dkt. Samia katika kuendeleza mageuzi ya sekta ya elimu, kukuza maendeleo ya rasilimali watu, pamoja na kuimarisha diplomasia ya Tanzania na hadhi ya nchi katika jukwaa la kimataifa.


Mhe. Dkt. Samia ametunukiwa heshima hiyo wakati wa ziara yake rasmi nchini Urusi, kufuatia mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Mhe. Vladimir Putin. Tuzo hiyo pia inatambua mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuvutia uwekezaji, na kuitangaza Tanzania duniani kupitia sekta mbalimbali za maendeleo, ikiwemo utalii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso