NYAKANYENGE AONGOZA MAPOKEZI YA KATIBU HAPI SHINYANGA, ZIARA YA SIKU MBILI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 4 June 2026

NYAKANYENGE AONGOZA MAPOKEZI YA KATIBU HAPI SHINYANGA, ZIARA YA SIKU MBILI.


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wazazi, CCM Taifa , Edwin Nyakanyenge, ameongoza mapokezi ya Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Ally Hapi, alipowasili Mkoani Shinyanga Juni 4, 2026.


Hapi ameanza ziara yake ya siku mbili mkoani hapa, Juni 5, 2026 anatarajia kutembelea Wilaya ya Kishapu.


Akizungumza mara baada ya mapokezi, Katibu Hapi amesema lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha uhai wa jumuiya na chama, pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.


Aidha, kiongozi huyo wa kitaifa amewataka viongozi wote walio na dhamana ya chama na serikali kuwa mstari wa mbele katika kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati.


Kwaupande wake Nyakanyenge mjumbe kamati ya utekelezaji wazazi CCM Taifa ameahidi ushirikiano wa viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga ili ziara hiyo ifanikiwe na wananchi wapate majibu ya kero zao.


Ziara hiyo inatarajiwa kukamilika Juni 5 baada ya viongozi hao kutembelea na kuzungumza na wananchi wa Kishapu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso