DC NKINDA AWAONYA WAZAZI KUWADHIBITI WATOTO DHIDI YA USHIRIKI WA MAANDAMANO YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA JULAI 7 NA AGOSTI 8 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 21 June 2026

DC NKINDA AWAONYA WAZAZI KUWADHIBITI WATOTO DHIDI YA USHIRIKI WA MAANDAMANO YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA JULAI 7 NA AGOSTI 8

 

Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Vituo vya Maendeleo ya Mtoto na Kijana Klasta ya Kahama yaliyofanyika katika kanisa la FPCT Shalom Temple.

Na Neema Nkumbi, Kahama


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawasimamia na kuwadhibiti watoto wao ili wasijihusishe na maandamano yanayotarajiwa kufanyika nchini tarehe 7 Julai na 8 Agosti mwaka huu, akieleza kuwa usalama na ustawi wa watoto ni jukumu la familia na jamii kwa ujumla.

Nkinda ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kanisa la FPCT Shalom Temple mjini Kahama, ambapo amesisitiza kuwa watoto wanapaswa kuelekezwa kwenye masuala ya elimu, maadili na maendeleo yao badala ya kuingizwa katika shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama wao.

Amesema wazazi na walezi wana wajibu mkubwa wa kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuhakikisha hawashawishiwi au kutumiwa katika shughuli ambazo zinaweza kuwaweka katika mazingira ya hatari.

"Ninatoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao ipasavyo, Watoto wanapaswa kulindwa na kupewa malezi bora, si kuingizwa katika shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama na mustakabali wao," amesema Nkinda.

Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia sheria na taratibu zilizowekwa kwa lengo la kulinda amani, usalama na maslahi ya watoto pamoja na wananchi kwa ujumla.

Aidha, amewataka viongozi wa jamii, taasisi za dini na wadau wa maendeleo ya watoto kuendelea kutoa elimu kwa watoto na vijana kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria, maadili na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso