WAGOMBEA 8 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI MDOGO KATA YA ZONGOMERA, KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 4 May 2026

WAGOMBEA 8 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI MDOGO KATA YA ZONGOMERA, KAHAMA


Na Neema Nkumbi, Kahama


Wagombea nane (8) wanaowakilisha vyama mbalimbali vya siasa leo may 4, 2026 wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya uongozi katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Zongomera, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Majina ya wagombea hao ni Machibya Omary Shija (Chama Cha Mapinduzi - CCM), Mohamed Msanya Msanya (Chama cha makini), Meshack Deus Masuguliko (Chama cha NLD), Monika Paul Masunga (Chama cha AAFP), Paul Richard Seleli (TLP), Julius Venance Bulilo (SAU), James Paul Frank (CHAUMMA) pamoja na Neema Kasim Yegeyege (UMD), wote wakitokea kata ya zongomera.

Zoezi la uchukuaji wa fomu limefanyika katika ofisi za kata ya zongomera manispaa ya kahama kwa utaratibu mzuri na amani, huku wagombea na wadau wa siasa wakizingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyama vinavyoshiriki, hali inayoashiria kukua kwa demokrasia katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso