RIPOTI YA JAJI CHANDE: BABY MADAHA AFUNGUKA MAZITO, ACHAGIZA UWAJIBIKAJI KUPONYA TAIFA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 7 May 2026

RIPOTI YA JAJI CHANDE: BABY MADAHA AFUNGUKA MAZITO, ACHAGIZA UWAJIBIKAJI KUPONYA TAIFA


Mwanadada Baby Madaha, ambaye si tu ni msanii mwenye historia ndefu, bali pia ni mdau aliyeshiriki kikamilifu katika kutoa ushahidi mbele ya tume Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ameeleza kuridhishwa kwake na weledi uliotumika katika kuchunguza matukio hayo na kuleta rejea kwa Watanzania.

Amesema ameikubali ripoti hiyo ya Mheshimiwa Jaji Mohamed Chande Othman kwani imeonesha jinsi alivyotumia uzoefu na weledi mkubwa katika masuala ya sheria, haki za binadamu na utunzaji wa amani kusaidia taifa kupata njia ya uponyaji .

Jaji Chande ambaye amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuanzia mwaka 2010 hadi 2017, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amewahi kushiriki kama mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa katika Uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Lebanon na Sudan. Aidha amewahi kuwa Mjumbe wa Timu ya Kupitia Sheria iliyoanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC.

Amewahi pia kuwa mjumbe wa Timu huru ya wataalamu ya kutathmini utendaji na ufanisi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, amewahi kuwa mwendesha mashtaka mkuu katika kesi za uhalifu uliotokea nchini Timol Mashariki, amewahi kuwa mwendesha mashtaka katika mahakama ya umoja wa mataifa ya uhalifu wa mauaji wa Rwanda, Pia alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Rais ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini

Baby Madaha,ambaye alishiriki kutoa ushahidi upande wa wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), amebainisha kuwa ripoti hiyo imekidhi vigezo vyote vya ukamilifu na imejibu kiu ya wananchi waliokuwa na maswali mengi yasiyo na majibu.

“Nimepokea vizuri ripoti imekamilika na imekidhi vigezo vyote vya kuwa kamili. Ina majibu ya maswali yote yaliyokuwa yanaulizwa na wananchi kuanzia kina nani walichagiza vurugu hizo, chanzo ni nini, walikuwa na lengo gani, athari zipi zimetokea na nini kifanyike kuponya taifa,” alisema Baby Madaha kwa msisitizo.

Kwa mujibu wa Baby Madaha huu ni wakati wa vitendo na si maneno pekee na ni lazima wale wote waliotajwa kuchagiza vurugu hizo wawajibike kwa mujibu wa sheria.

“Nikiwa kama mtu niliyeshiriki kikamilifu katika mahojiano na tume kwa upande wa wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, nadhani ni wakati sasa wa vyanzo hivyo kuwajibika na walichokichagiza,” aliongeza, akionyesha msimamo usioyumba kuhusu haki na uponyaji wa kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso