WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA MAALUMU TCRA, APOKELEWA NA UONGOZI WA MAMLAKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 25 November 2025

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA MAALUMU TCRA, APOKELEWA NA UONGOZI WA MAMLAKA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.) amepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari, alipowasili katika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam tarehe 25 Novemba, 2025, kwaajili ya ziara maalumu.


Mhe. Kairuki ameambatana na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholaus Merinyo Mkapa, pamoja na watumishi wengine wa Wizara.


Katika ziara hiyo ya siku moja, Mhe. Waziri atapokea mawasilisho mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TCRA kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu pamoja na Wakurugenzi wa Idara.

#tcratz #ziaratcra

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso