WATANZANIA KATAENI KUVURUGWA DESEMBA 9 – AMANI NDIO RIZIKI YETU! - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 20 November 2025

WATANZANIA KATAENI KUVURUGWA DESEMBA 9 – AMANI NDIO RIZIKI YETU!


Katika hali inayoonyesha wasiwasi wa baadhi ya wananchi kuhusu mipango ya uvunjifu wa amani, inayosambazwa mitandaoni hasa ile inayoelezwa kulenga Desemba 9, wito umetolewa kwa Watanzania wote kusimama imara na kukataa ushawishi wa wale wanaotaka kuingiza taifa kwenye machafuko.

Wananchi wamesema amani ni msingi mkuu wa maisha yao ya kila siku, huku wakisisitiza kwamba hakuna kazi wala maendeleo yanayoweza kupatikana bila utulivu.


Amani Huratibu Kazi, Huzima Vurugu

Malugu Nkwabi mkazi wa Bariadi ambaye ni Afisa Usafirishaji, alitoa msisitizo mkubwa kwa umuhimu wa amani katika ufanisi wake wa kazi.


"Ni lazima Watanzania tushikane kuhakikisha amani ndiyo kila kitu. Amani ndiyo kitu cha muhimu sana kwenye taifa. Maisha yote yanategemea kuwepo kwa amani. Ukiangalia kuanzia saa 12:00 jioni ukifika ni lazima nifanye kazi ili niweze kurudi nyumbani na maisha yangu kuendelea. Huwezi kufanya kazi pasipo kuwepo amani.."


Kauli hii inalenga moja kwa moja wale wanaofikiria kuandamana au kufanya vurugu, ikiwakumbusha kwamba uvunjifu wa amani kwanza unakwenda kuathiri shughuli zao za kujipatia riziki.


Kwa upande wake, Bwana Marco Mahega,kutoka mkoani Simiyu , alieleza masikitiko yake kwa jinsi Watanzania wanavyotaka kuichoma nchi yao na kukumbusha nchi zenye migogoro, akisisitiza kuwa amani inalinda hata viwango vya chini vya jamii.


"Sisi wenye familia zetu tukikuta nchi haina amani hatuna kwa kuikimbilia... Tunashukuru Mwenyezi Mungu, tumepewa amani. Naomba tuendelee kuihifadhi. Ukiona nchi haina amani maana yake haina amani hata kwenye familia yako. Tunaangalia nchi nyingi ambazo hazina amani wanatumia muda wao mwingi kuendelea kwenye migogoro. Sisi amani ndiyo kila kitu. Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kudumisha amani."


Wakati wakikataa vurugu, wananchi pia wanatoa wito kwa viongozi kuwajibika. Bwana Paul Mboyi,alielekeza wito wake kwa viongozi waliochaguliwa hivi karibuni, akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi badala ya kuendeleza siasa.


"Kila mtu atimize wajibu wake... Naomba viongozi ambao kwanza wamechaguliwa waanze kufanya yale mambo waliyoahidi. Tusiishie tu kwenye siasa. Tunaomba viongozi kuwafuata wananchi, wasikae ofisini tu. Mkutano wa mkoa tulinde kwanza kauli ya amani. Kusiwe na makundi."


Wito wa Bwana Mboyi unaonesha kuwa wananchi wanataka kuona uongozi unajikita katika maendeleo, lakini wanakiri kwamba amani lazima ilindwe kwanza kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso