Njama za kuratibu vurugu za kitaifa zilizolenga kuzuia uchaguzi mkuu na hatimaye kuipindua Serikali zimefeli vibaya, huku vyama 17 kati ya 19 vilivyoshiriki uchaguzi vikidaiwa kujitenga na mipango hiyo. Mtoa taarifa wetu amedai kuwa, hatua hii imewaacha waratibu wakuu,wakiwa katika wakati mgumu.
Inadaiwa kuwa waratibu hao wamekasirishwa sana na kushindwa kwa njama yao ya kumtoa madarakani Rais wa Tanzania aliyechaguliwa kidemokrasia, baada ya zoezi hilo kufeli licha ya kugharimu fedha nyingi kutoka kwa wafadhili wa kitaifa na kimataifa.
Mtoa taarifa anasema mratibu mmoja ambaye anadaiwa kuweka kambi ya kuratibu vurugu za kupindua Serikali, aliingiza vijana wengi kutoka nchi jirani kuja kuwafundisha Watanzania fujo. Vijana hao walidaiwa kuingia nchini kupitia njia za panya na kubebwa kwenye magari hadi kwenye maeneo yaliyoanzia vurugu.
Inadaiwa kuwa Commander in Chief na master mind wa vurugu hizo, akitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu zilizosababisha mauaji na uharibifu yupo kwenye wakati mgumu kwa kuwa jeshi lake la mchongo lililohusisha vijana wa fujo wasiokuwa na kazi kutoka nchi jirani limeangamizwa... Wazazi wa hao vijana sasa wanamtaka awarudishe vijana wao ambao kwa tamaa ya pesa walifika Tanzania kufanya uhalifu.
Vurugu zilizoratibiwa, ambazo CHADEMA inatajwa kuwa muasisi wake kwa kutangaza kuwa uchaguzi hautofanyika, zilisababisha,mauaji ya Polisi na raia,wizi na uporaji,kuteketeza kwa moto miundombinu ya usafiri, hospitali, ofisi za TRA, shule, na miundombinu ya biashara za watu.
Vyombo vya ulinzi na usalama vililazimika kutumia risasi za moto kudhibiti wezi, waporaji na waharibifu ili kuzuia nchi isiteketezwe na moto uliowashwa sehemu mbali mbali.
Mtoa taarifa alimalizia kwa kusema kuwa maafa yaliyotokana na vurugu hizi hayapaswi kuachiwa kujirudia.

No comments:
Post a Comment