WAKILI UKASHU ASISITIZA MUAFAKA, AUNGA MKONO DIRA YA RAIS SAMIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 15 November 2025

WAKILI UKASHU ASISITIZA MUAFAKA, AUNGA MKONO DIRA YA RAIS SAMIA


Na Mwandishi Wetu


Hatua za Serikali za kuunda Tume Maalumu ya kuchunguza vurugu zilizotokea nchini zimepokelewa kwa matumaini na wachambuzi, huku wakisisitiza kuwa jukumu la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama "Comforty Mkuu" wa Taifa ndilo litaleta uponyaji wa kweli.

Wakili na Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii, Emmanuel Ukashu, ameeleza kwamba hotuba ya Rais Samia ya kufungua Bunge la 13 imetoa mwelekeo bora kabisa wa uponyaji wa Taifa katika majira haya magumu.

Akichambua hali ya kisiasa kabla na baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025, Wakili Ukashu alifafanua:“Unajua kilichotokea ni matokeo lakini tayari huko nyuma haya mambo yalikuwa yanaonywa, kwa sababu tumepitia nyakati ngumu kama Taifa. Nchi imevimba, na nchi ili iweze kuwa na muafaka lazima watu tukae chini tuzungumze,” alisisitiza Wakili Ukashu.

Anasisitiza kuwa hotuba ya Rais imekuwa muhimu sana kwa sababu inalenga kuleta muafaka wa kitaifa unaoanza kwa Taifa kujitambua na kujitegemea kifikra, kisha kuunda mazingira ya mazungumzo.

Rais Samia: “Comforty Mkuu” wa Taifa

Kwa Wakili Ukashu, katika nyakati ambazo Taifa limepitia wakati mgumu, Rais Samia ndiye amekuwa comforty mkuu (mfariji mkuu), ambaye hotuba yake imetoa mwelekeo wa uponyaji.

Katika hotuba yake, Rais Samia alitoa wito wa maridhiano na umoja, akiahidi kuendelea kunyoosha mkono kwa wadau wa kisiasa. Alitangaza kuwa Tume Maalumu imeundwa kuchunguza chanzo cha vurugu hizo na kwamba ripoti yake itatumika kama mwongozo wa hatua za kuelekeza Taifa kwenye amani ya kudumu. Pia, alitoa msamaha kwa vijana waliofuata mkumbo wa uhalifu.

Hatua hizi za Rais, hasa uundwaji wa Tume ya Uchunguzi, zinalenga kutibu majeraha ya kijamii na kuimarisha misingi ya amani, sambamba na kuheshimu utu wa kila Mtanzania.

Ushauri wa Tume ya Maridhiano

Kama sehemu ya mwelekeo wa uponyaji wa taifa, Wakili Ukashu alishauri kwamba mbali na Tume ya uchunguzi, Taifa linahitaji Tume ya Maridhiano .

Alipendekezi kuwa tume ya uchgunguzi inafaa majaji kuwepo, ipewe muda wa kutosha wa kufanya utafiti wa kina kuhusu kiini cha vurugu hizo na taarifa yake iwekwe wazi kwa umma ili kuanzisha misingi ya uwazi na uwajibikaji.

Mapendekezo ya Wakili Ukashu yanaonekana kuendana na dhamira ya Rais Samia ya kuanza mchakato wa Katiba Mpya kwa kuanzisha Tume ya Usuluhishi na Maelewano, ikionyesha Serikali iko tayari kukaa chini kuzungumza na wadau wote.

Kwa ujumla, wachambuzi wanaona hotuba ya Rais Samia imefungua ukurasa mpya wa maridhiano, uwazi, na uponyaji, huku ikisisitiza kuwa safari ya kuelekea amani ya kudumu inahitaji ushiriki wa kila Mtanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso