ARUSHA INANG'ARA TENA: WATANZANIA WAKAZIA AMANI, WAUPUUZA UPOTOSHAJI BAADA YA VURUGU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 11 November 2025

ARUSHA INANG'ARA TENA: WATANZANIA WAKAZIA AMANI, WAUPUUZA UPOTOSHAJI BAADA YA VURUGU



Kufuatia matukio ya hivi karibuni ya uchafuzi wa amani na uharibifu wa mali huko Arusha, Watanzania wameungana na kutoa wito wa kitaifa wa kurejea kwenye hekima, upendo na umoja, huku wakikataa vikali vitendo vya vurugu.


Ingawa vituo vya mafuta viliungua, ofisi ziliharibiwa, na biashara kusimama kwa muda, jiji la Arusha sasa limesimama tena, likisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo.


Akizungumzia hali ya mji huo, Josephat Akiiro, alisema kuwa Arusha imeonyesha ukomavu baada ya changamoto:


"Vituo vya mafuta vimeungua. Ofisi zimeharibiwa. Biashara zimesimama. Lakini leo, Arusha imesimama tena, kama jiji la hekima, umoja, na matumaini."


Akiunga mkono kauli hiyo, Mwananchi wa Arusha mjini, Hanifa alisisitiza kuwa vurugu haina nafasi:




"Vurugu haina faida, bali amani ndiyo msingi wa maendeleo na heshima ya taifa. Tuchague amani, tujenge tena. Kwa Arusha. Kwa Tanzania."




"Watanzania, Upendo Ndio Dira Yetu! Tujenge Daraja la Upendo linalounganisha kabila, dini, na itikadi zetu... Tupendane, tuheshimiane, na tushirikiane kwa moyo mmoja ili Tanzania iendelee kung'ara. Amani yetu ni urithi wetu, tuulinde kwa Upendo!" alisema


Kwa upande wake, Bi. Latifa Merinyo alisisitiza kuwa wanapaswa kuepuka upotoshaji,tulinde tunu ya amani kwa maendeleo ya nchi.


Bi Latifa alisema hayo huku akikariri, maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisema:"Ukiona mtu anataka kuharibu amani ujue anaujihumu uhuru wetu. Tusikubali kutumiwa kuvuruga tulichokijenga kwa miaka mingi."


Wananchi wengi waliohojiwa wamehimiza kuendelea kulinda amani na mali za umma, wakisisitiza kwamba "Uchafuzi wa Amani sio Desturi za Mtanzania" na kwamba "Amani Yetu, Fahari Yetu."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso