USIKU WA WADAU SHUPAVU MKOA WA SHINYANGA KUFANYIKA LEO ZAKARIA HALL - KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 17 October 2025

USIKU WA WADAU SHUPAVU MKOA WA SHINYANGA KUFANYIKA LEO ZAKARIA HALL - KAHAMA





SHINYANGA, Oktoba 17, 2025 


 Ni siku ya furaha na historia kwa wadau wa maendeleo mkoani Shinyanga, ambapo leo inafanyika hafla maalum ya “Usiku wa Wadau Shupavu Mkoa wa Shinyanga – Msimu wa Kwanza” katika ukumbi wa Zakaria Hall, mjini Kahama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mdau Shupavu Mkuu, Sir Bweichum, maandalizi yote yamekamilika na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya mkoa huo wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo lililoandaliwa kwa lengo la kutambua, kuthamini na kuunganisha wadau wanaochangia maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali.



“Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wote ambao tayari mmefanikisha kununua tiketi kwa ajili ya tukio hili letu muhimu. Kama taasisi, hatuna cha kuwalipa zaidi ya kutambua na kuthamini kwa moyo wote michango yenu ya dhati,” amesema Sir Bweichum kupitia ujumbe wake wa shukrani kwa wadau.

Ameongeza kuwa ushirikiano ulioonyeshwa na wadau katika maandalizi ya tukio hilo ni kielelezo cha umoja na mapenzi kwa maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga, akiwataka washiriki wote kuendelea kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

“Karibuni sana leo hapa Zakaria Hall, mahali ambapo kila mdau ni muhimu, kwa sababu hafla hii ni ya watu na watu hao ni ninyi wadau wetu shupavu.”

Hafla hiyo inatarajiwa kuvuta wadau kutoka sekta za serikali, mashirika binafsi, vyombo vya habari, taasisi za kijamii na vijana wabunifu, huku ikipambwa na burudani, tuzo na maonyesho ya mafanikio ya wadau shupavu wa mkoa huo.

Kwa mujibu wa waandaaji, lengo kuu la hafla hiyo ni kujenga mtandao imara wa wadau wa maendeleo, kuhamasisha ushirikiano na kuonyesha mchango wa watu binafsi na taasisi katika kubadilisha taswira ya Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso