Tahadhari kwa Wahamasishaji na washiriki wanaotaka kuharibu uchaguzi mkuu
Na Mwandishi wetu
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayejaribu kuandaa maandamano au uchochezi wa kihalifu.
"Anayetaka kuandamana atakamatwa, ikiwamo wahamasishaji kama wataonekana," msemaji alieleza. Aliongeza kuwa Polisi inatambua wahamasishaji wengi, hata wale ambao 'kwa kawaida hujificha.'
Katika utekelezaji wa sheria, Polisi imesisitiza kuwa mbinu za kiteknolojia zimeimarishwa. "Tunajua wametengeneza majina bandia feki, lakini katika ulimwengu huu wa teknolojia huwezi kujificha," alisema.
Alifichua kuwa vifaa vya kielektroniki vinawasaidia kuwafuatilia hata wale ambao wanadhani wamejificha.
Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi David Misime alisema kwamba ni muda tu ukidhani kwamba unachoichea halafu hushiriki hatutakukamata unajidanganya ni muda tu.
Hata hivyo, Polisi ilisisitiza kuheshimu haki ya kupiga kura. "Kama unaonekana unapita kwenda kupiga kura, na tunakujua ni mmoja ya wachochezi tutakuacha upige kura," alisema na kuongeza, "Tutakusubiri ukimaliza, ndipo tutakukamata. Si unakosa la jinai?" Kauli hii inatoa taswira kwamba Polisi itaweka kipaumbele katika usalama wa uchaguzi huku ikihakikisha sheria inafuatwa kwa wale wanaotenda makosa ya jinai wanakamatwa
Kuhusu utoaji wa taarifa, msemaji huyo alikanusha madai ya waandishi wa habari kwamba hakuna kinachofanyika. "Kila mara Polisi wanatoa taarifa kwa umma... yapo mengi tunayofanya, waandishi naapaswa kukumbushia haya ambayo ni mwendeleo" alisema, akisisitiza kwamba Polisi huhakikisha ufumbuzi wa mashauri tata na magumu unapatikana.
Aidhanmsemaji wa Polisi alihimiza jamii kuanzia kwenye kiwango cha familia kushughulikia matatizo kabla hayajawa uhalifu. "Tusitupiane mpira," alisema. "Tuanzie katika familia. Wanaodhulumiana, wapenzi kuoneana wivu na ushirikiana," aliongeza.

No comments:
Post a Comment