Na, Mwandishi wetu, Kelvin Nandwa - Nairobi.
Hali ya taharuki imeendelea kushuhudiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi baada ya ucheleweshwaji wa kuondoka kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Raila Amolo Odinga.
Vijana na wafuasi wake walikusanyika kwa wingi nje ya uwanja huo, wakishinikiza mwili huo kupelekwa moja kwa moja Uwanja wa Kasarani kwa ajili ya wananchi kuuaga, badala ya kupitishwa kwenye njia ya siri kupitia Expressway kama ilivyopendekezwa na maafisa wa usalama.
Jeshi la Ulinzi la Kenya lilipanga kuusafirisha mwili huo kwa ndege, lakini wafuasi wamekataa, wakisisitiza mwili upelekwe Uwanja wa Kasarani kwa ajili ya kuagwa na umma.
Wakati huo huo, Bunge la Taifa linaendelea na kikao maalum cha kutoa heshima kwa aliyekuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani.
Ikumbukwe kuwa Hayati Raila Odinga alizaliwa mwaka 1945 katika familia yenye historia ya kisiasa, na inaelezwa kuwa alianza siasa mapema na kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani nchini Kenya, akipigania demokrasia na uwajibikaji wa serikali.
Odinga aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya kutoka 2008 hadi 2013 na alikuwa kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM). Kwa karne moja, Raila alikuwa sauti ya wafuasi wake kwa ajili ya haki, maendeleo ya kijamii, na mabadiliko ya kisiasa, Kifo chake kimeacha pengo kubwa kisiasa na kihisia na likitafsiriwa kama kuondoka kwa kiongozi aliyeathiri historia ya kisiasa ya Kenya.
Hatahivyo, mwili wa Hayati Raila Odinga tayari umeshafikishwa katika Uwanja wa Kasarani, tayari kwa taratibu za kuaga huku umati wa watu ukiendelea kujaa kwa maelfu ya wafuasi, wakiongozwa na viongozi wa ODM na serikali kwaajili ya kutoa heshima za mwisho na kushuhudia kuaga taifa.
Mamia ya wafuasi wa Raila Odinga wameingia JKIA ili kupokea mwili wake kutoka India
No comments:
Post a Comment