JAJI MWAMBEGELE ATEMBELEA WILAYA YA CHAMWINO KUKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2025 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 25 September 2025

JAJI MWAMBEGELE ATEMBELEA WILAYA YA CHAMWINO KUKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2025


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia mabegi kwaajili ya mafunzo kwa watendaji wa vituo wakati wa Uchaguzi wakati alipotembnelea ghala la vifaa vya Uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana. Jaji Mwambegele pia alitembelea Halmashauri za Wilaya ya Bahi na Dodoma Mjini mkoani humo kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia bango mshale ambalo hutumika kuelekeza wapiga kura katika vituo ya kupigia Kura wakati alipotembnelea ghala la vifaa vya Uchaguzi katika Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma jana. Jaji Mwambegele pia alitembelea Halmashauri za Wilaya ya Bahi na Dodoma Mjini mkoani humo kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025.


***


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 25, 2025 ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma katika majimbo ya Chamwino na Mtera ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.


"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso