CHEREHANI EMMANUEL ACHUKUA FOMU YA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU KUPITIA CCM - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 24 August 2025

CHEREHANI EMMANUEL ACHUKUA FOMU YA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU KUPITIA CCM




Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ushetu, Wilaya ya Kahama, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Cherehani Emmanuel , leo Agosti 24, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.


Cherehani ambaye aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa kupeperusha bendera ya chama hicho amepokelewa na kukabidhiwa fomu hiyo na Afisa Uchaguzi katika Jimbo hilo Charles Mburu.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu, Cherehani amekishukuru Chama chake na wananchi kwa imani waliompa huku akisisitiza mshikamano ndani ya chama na kuondoa makundi ya makambi ili kujenga Ushetu yenye mshikamano na maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso