Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga limewakamata jumla ya watu 125 wanaotuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali ya kihalifu, ikiwemo usambazaji wa dawa za kulevya na wizi wa mali, katika kipindi cha kuanzia juni hadi julai 22, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 23, Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga, sacp janeth magomi, amesema ukamataji huo ni matokeo ya operesheni maalum zinazoendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
"Katika operesheni hizi, tumefanikiwa kukamata dawa za kulevya zikiwemo bhangi gramu 2,261, mirungi kilo 29 na pombe ya moshi lita 142," amesema kamanda magomi.
Aidha, vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 22 ambazo baadhi nimali za qizi na zingine hazina usajili, bajaji moja, mabati 16, nondo 17, vitanda vinne na redio nane.
Kamanda magomi ameongeza kuwa juhudi hizo ni sehemu ya mikakati ya jeshi la polisi kuhakikisha jamii inakuwa salama na huru dhidi ya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa wananchi kwa kutoa taarifa kuhusu wahalifu na vitendo viovu vinavyofanyika katika maeneo yao, ili kusaidia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment