JAJI MWAMBEGELE: SIMAMIENI MAADILI NA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA UCHAGUZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 23 July 2025

JAJI MWAMBEGELE: SIMAMIENI MAADILI NA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.

NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL SHINYANGA

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufani Mheshimiwa Jacobs Mwambegele, amewataka watendaji wa uchaguzi kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia uchaguzi nchini.

Akifunga mafunzo maalum kwa Waratibu wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Majimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ununuzi, Jaji Mwambegele amesema kuwa ni wajibu wa watendaji hao kufikisha elimu kwa weledi kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata pamoja na watendaji wa vituo vya kupigia kura.

"Simamieni vema matumizi ya fedha mtakazotumiwa kwa ajili ya shughuli za uchaguzi, Vifaa vya uchaguzi vikishapokelewa, hakikisheni mnakuwa na orodha kamili na iwapo kuna upungufu toeni taarifa kwa Tume mapema,” amesisitiza Jaji Mwambegele.

Amesisitiza pia umuhimu wa usimamizi makini wa rasilimali zote, kuhakikisha vifaa vya uchaguzi vinatumiwa kwa ufanisi na kufanya uhakiki kabla ya kuanza kutumika, Vilevile, amewakumbusha watendaji hao kuwa makini na taarifa wanazotoa kwa vyombo vya habari.

“Iwapo mtatakiwa kutoa taarifa kwa umma au kwa vyombo vya habari, hakikisheni taarifa hizo zimehakikiwa ili kuepusha taharuki kwa wananchi na taifa kwa ujumla,” ameongeza Jaji Mwambegele.

Katika kuhakikisha uwazi na haki katika uchaguzi, amewataka watendaji kuhakikisha mabango, matangazo na orodha ya wapiga kura yanabandikwa katika maeneo yote yanayopaswa kufikiwa na wananchi, kama inavyotakiwa kisheria.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Faustine Lagwen, amesema kuwa washiriki wa mafunzo hao wako tayari kusimamia uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

“Jumla ya mada 12 zimewasilishwa katika mafunzo haya ili kuwawezesha watendaji wa uchaguzi kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi,” amesema Lagwen.

Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso