VIONGOZI WA DINI mbalimbali nchini, wameshauriwa kuwa mhimili wa kulinda amani ya NCHI kwa kuhamasisha waumini wao kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi Bora .
Hayo yalielezwa na Mwezeshaji wa semina ya siku mbili , Maftah Ng'webwya Maftah kutoka Taasisi inayoundwa na dini mbalimbali ya Interfaith, iliyofanyika wilayani Kahama, ambapo alisema viongozi wa dini Wana wajibu mkubwa wa kupigania amani ya nchi hii
Maftah alisema viongozi wa dini ni watu muhimu katika amani ya nchi, kwakuwa wamejaaliwa karama kubwa ya ushawishi kwa waumini , na kutakiwa kuwa mistari wa mbele kuhamasisha wananchi wajitokeze kupiga kura kupata viongozi Bora wenye maono ya maendeleo ya Taifa letu.
Alisema Chaguzi za Afrika Zina madhaifu lakini wametakiwa kuendelea kuitangaza amani ya nchi katika nyumba za Ibada, huku wakitafuta njia rafiki ya kukabiliana na madhaifu hayo kwa kushauriana na serikali.
Nae Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA ) wilaya ya Kahama, Haji Nasser Amary, alisema hakuna haja ya kususa Chaguzi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhalalisha kupatikana kiongozi asiyefaa.
Kwa upande wake Padre Anold Toyi kutoka Parokia ya Mbogwe, alisema mfumo wa nchi yetu ni wagombea kubwa na vyama hivyo wananchi wanatakiwa kuangalia sera Bora na kiongozi anayestahiki ili kuwavusha katika suala la maendeleo.
No comments:
Post a Comment