TCRA: WAANDISHI 254 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SAMIA KALAMU AWARDS, AI YATAJWA KUIMARISHA UANDISHI WA HABARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 6 May 2025

TCRA: WAANDISHI 254 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SAMIA KALAMU AWARDS, AI YATAJWA KUIMARISHA UANDISHI WA HABARI

 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amesema mchakato wa maandalizi ya tuzo za Samia Kalamu Awards yamewezesha Waandishi wa Habari 254 kupata elimu kuhusiana na masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi na ubora wa kazi za waandishi.

7
Akitoa taarifa ya TCRA kama Muandaaji mwenza wa Tuzo hizo, Dkt. Jabiri amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) walifanya utafiti na kugundua kuwa wanahabari wengi wanakosa sifa ya kutambua habari muhimu zinazohusiana na maendeleo na ndio maana wakaanzisha mafunzo hayo.


Amesema mafunzo hayo yalifanyika kwa waandishi wa Habari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na baada ya mafunzo hayo wameona mabadiliko makubwa katika kazi za Uandishi na taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya Habari.




Amesema, moja ya eneo ambalo wameligusia kwenye mafunzo hayo ni matumizi ya Akili unde (AI) na uandishi wa Habari zenye tija kwa manufaa ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso