RAIS SAMIA: UHURU WA HABARI UENDANE NA UZALENDO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 6 May 2025

RAIS SAMIA: UHURU WA HABARI UENDANE NA UZALENDO


Rais Samia Suluhu Hassan amewataka waandishi wa Habari na vyombo vya Habari kwa ujumla kuutumia Uhuru wa vyombo vya Habari kuhabarisha Umma lakini kuweka na Uzalendo wakati wakifanya kazi zao.


Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Samia Kalamu Awards, Rais Samia amesema, jambo ambalo ameahidi mara kwa mara kwa wanahabari ni kukuza Uhuru wa vyombo vya Habari jambo ambalo linaonekana wazi.


Rais Samia amesema, Uhuru wa Habari uliopo uendelee kuwa chachu kwa wanahabari lakini lazima Uhuru huo uendane na Uzalendo wanapotoa Habari kwa jamii.


Amewataka Waandishi wa Habari, kutumia Takwimu kutoa taarifa zao kwani uandishi wa kutumia takwimu una manufaa makubwa kwa jamii na unatoa nafasi kubwa kwa jamii kuona maendeleo yanayofanywa na Serikali.


Kuhusu matumizi ya Lugha sanifu ya Kiswahili, Rais Samia amewataka waandishi wa Habari kutumia lugha vizuri ili taarifa wanazozitoa zieleweke na pia kukuza lugha hiyo hapa nchini na ulimwenguni kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso