KATIBU MKUU MHA. CYPRIAN LUHEMEJA AFUATILIA ZOEZI LA USAFISHAJI WA ZIWA VICTORIA KATIKA ENEO LA BUSISI – KIGONGO FERI, MWANZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 16 May 2025

KATIBU MKUU MHA. CYPRIAN LUHEMEJA AFUATILIA ZOEZI LA USAFISHAJI WA ZIWA VICTORIA KATIKA ENEO LA BUSISI – KIGONGO FERI, MWANZA



Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mha. Cyprian Luhemeja akifuatilia zoezi la usafishaji Ziwa Victoria katika eneo lililoathirika na Gugu Maji eneo la Busisi wilayani Sengerema hadi eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Mei 15, 2025.


Zoezi hilo linaendelea kufanyika kwa njia mbalimbali kupitia vijana wanaokata kwa kutumia panga pamoja na Mtambo wa kusafisha na kuchimba kina cha maji ‘Watermaster’ ambao unauwezo wa kusafisha eka moja kwa siku.


Wakati zoezi hilo likiendelea tayari hatua zaidi zimeendelea kuchukuliwa ikiwa pamoja na ununuzi wa mitambo mitatu ambayo ipo katika hatua za awali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso