Na Paul Kayanda Mbogwe
MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita Nicodemus Maganga leo ameumgana na wananchi wa jimbo hilo na kushiriki la kupiga kura kwa lengo la kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza kwenye ngazi za serikali ya kijiji na vitongoji .
Maganga amepiga kura hiyo katika kutuo kilichopo shule ya sekondari Masumbwe huku akipongeza kwa namna zoezi hilo linavyokwenda na wananchi wanavyojitokeza na kudumisha amani na utulivu.
Mbunge Maganga ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura ambapo amesisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwenye vituo mbalimbali ili kutimiza haki yao ya msingi ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi watakao wafaa .
"Nikweli ndugu za waandishi kama mnavyojua leo nisiku ya mapumziko kwa nchi nzima kwa lengo la kupiga kura ili wananchi waweze kupata viongozi watakao watumikia na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.hivyo mimi kama mbunge nami nimeshapiga kura "amesema Maganga .
Hata hivyo Mbunge Maganga amepongeza wananchi wake kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu katika kipindiki hichi cha uchaguzi nakwamba yeye kama mbunge ameweza kushiriki katika kampeni za kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kutumia kikamilifu uchaguzi kuchagua viongozi wanaowafaa hususani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM.
Amemaliza kwa kusema kuwa wananchi hao wajitahidi kuchagua viongozi wanaotokana na CCM ili kumrahisishia kutekeleza majukumu yake ya kibunge kwenye maeneo yao hasa katika kuwapelekea maendeleo na kwamba uchaguzi ndio unatoa sura ya maendeleo kwenye maeneo kwasababu sifa moja wapo ni kujua idadi ya waliopiga kura katika eneo husika .
Pia katika ziara zake za kuhamasisha wananchi kupiga kura alitumia mikutano hiyo kwa kuwataka wananchi kufanya siasa na huku wakifanya shughuli za kilimo ili kuweza kujinusuru na changamoto za kukosa chakula ,ambapo kama mbunge aliweza kugawa zana za kilimo kwa mabalozi wanaonatokana na Chama cha Mapinduzi CCM.









No comments:
Post a Comment