DC MHITA ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 27 November 2024

DC MHITA ASHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, akipiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika mtaa wa Igalilimi, kata ya Kahama mjini.

NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, ameshiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika mtaa wa Igalilimi, kata ya Kahama mjini.


Mhita amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani, huku akihakikishia umma kuwa hali ya usalama imeimarishwa.


"Hakuna kiashiria chochote cha uvunjaji wa amani, na hali ya utulivu inaendelea kutawala," amesema Mhita.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, ambaye ni msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Manispaa ya Kahama, ametaja kuwa jumla ya wapiga kura 320,000 wanatarajiwa kupiga kura katika vituo 312 vilivyopo katika halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Kibetu ameweka wazi kuwa maandalizi ya uchaguzi yamekamilika na wananchi wanahamasishwa kujitokeza kwa wingi.


Katibu tawala wa Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, amesema kuwa usalama wa uchaguzi umehakikishwa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.


Mbega amefafanua kuwa katika Wilaya ya Kahama, Halmashauri tatu zenye vituo 1,270 zinajipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na haki, bila ya kutokea kwa vurugu. "Tumejipanga kuhakikisha uchaguzi ni wa amani na haki," amesema Mbega.


Uchaguzi wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Kahama unaendelea vizuri, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa utulivu na usalama kwa ustawi wa demokrasia.

Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, Asema Halmashauri Zimejipanga Kudumisha Amani
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, akipiga kura

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, Atoa Rai kwa Wananchi Kuhusiana na Usalama na Amani katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, akipiga Kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika kituo cha shule ya msingi Nyahanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, Atoa Takwimu za Wapiga Kura
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, akipiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika katika mtaa wa Nyahanga

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Kahama, Joachim Simbila  akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Mhongolo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso